TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI UTUMISHI | VYUO NA AJIRA | Official site
Breaking News
Loading...

Monday, October 9, 2017

TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI UTUMISHI


JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA RAIS
SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA Kumb. Na. EA.7/96/01/J/49 07 Oktoba, 2017

TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI

Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Muhimbili National Hospital (MNH), Muhimbili Orthopaedic Institute (MOI), Government Chemistry Laboratory Agency (GCLA), Tanzania Forest Services (TFS), The Local Government Training Institute (LGTI), na Eastern Africa Statistical Training Centre (EASTC) anapenda kuwataarifu waombaji kazi wote walioomba kazi za Taasisi hizo kuwa usaili unatarajiwa kuendeshwa kuanzia tarehe 14-21 Oktoba, 2017 na hatimaye kuwapangia vituo vya kazi, waombaji kazi watakaofaulu usaili.
Wasailiwa wanaoitwa kwenye usaili wanapaswa kuzingatia maelekezo yafuatayo:-
i. Usaili wa Mchujo utafanyika tarehe 14 Oktoba, 2017 kama ilivyoainishwa kwenye tangazo, muda wa usaili umeainishwa kwa kila Kada
ii. Kila Msailiwa anapaswa kuwa na kitambulisho kwa ajili ya utambuzi.
iii. Vitambulisho vinavyokubalika ni pamoja na: Kitambulisho cha Mkazi, Kitambulisho cha Mpiga kura, Kitambulisho cha kazi, Kitambulisho cha Uraia au Hati ya kusafiria.
iv. Wasailiwa wanatakiwa kufika na Vyeti Halisi vya kuanzia kidato cha IV, VI, Stashahada, Stashahada ya Juu, Shahada na vyeti vya usajili wa bodi zao na kuendelea kutegemeana na sifa za Mwombaji alizonazo.
v. Wasailiwa ambao hawana Vyeti halisi na badala yake kuwasilisha “Testimonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati matokeo za kidato cha IV na VI (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA NA HAWATARUHUSIWA KUENDELEA NA USAILI.
vi. Kila msailiwa atajigharamia kwa chakula, usafiri na malazi.
vii. Kila Msailiwa azingatie tarehe na mahali alipopangiwa kufanya usaili.
viii. Kwa wale waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe Vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na mamlaka husika (TCU na NECTA)
ix. Waombaji kazi ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili watambue kuwa hawakukidhi vigezo. Hivyo wasisite kuomba tena pindi nafasi za kazi zitakapotangazwa

KUSOMA MAJINA HAYO ANGALIA HAPO CHINI
Download attachments:

google+

linkedin

About Author
  • BLOG NAMBA MMOJA KWA MATANGAZO YA AJIRA NA NAFASI ZA KAZI TANZANIA. Soma zaidi

    0 comments:

    POST A COMMENT