KUITWA KWENYE USAILI National Health Insuarance Fund | VYUO NA AJIRA | Official site
Breaking News
Loading...

Monday, May 8, 2017

KUITWA KWENYE USAILI National Health Insuarance Fund

TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI

Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya “National Health Insuarance Fund” (NHIF) inapenda kuwa taarifu watanzania wote walioomba kazi zilizokuwa zimetangazwa kwa niaba ya Mfuko huo kuwa, inatarajia kuendesha usaili na hatimaye kuwapangia vituo vya kazi waombaji wote watakaofaulu usaili huo.

Wasailiwa wanaoitwa kwenye usaili huo wanapaswa kuzingatiamaelekezo yafuatayo:-

1.Usaili utaanza saa moja kamili asubuhi (1:00) na utafanyika mahali na tarehe kama ilivyoanishwa katika jedwali hapo chini katika kila nafasi husika.

2.Kila Msailiwa atapaswa kufika na kitambulisho kwa ajili ya utambuzi vitambulisho vinavyotambulika ni pamoja na Kitambulisho cha Mkazi, Kitambulisho cha Mpiga kura, Kitambulisho cha kazi, Hati ya kusafiria, na Kitambulisho cha Uraia.

3.Kila Msailiwa atapaswa kufika na Vyeti Halisi (Original Certificates) vya kuanzia kidato cha IV, VI, Stashahada, Stashahada ya Juu, Shahada na kuendelea kutegemeana na sifa za Mwombaji.

4. “Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hatimatokeo za kidato cha IV na VI (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.

5. Sekretarieti ya Ajira haitahusika na gharama zozote zitakazotumiwa na wasailiwa katika kufanikisha kuhudhuria usaili huo.

6. Kila Msailiwa atapaswa kuzingatia tarehe na eneo alilopangiwa kufanya usaili.

7. Kila Msailiwa atapaswa kufika na cheti halisi cha kuzaliwa (Original Birth Certificate)

8. Kwa wale waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na mamlaka husika (TCU & NECTA) na watapaswa kufika na vielelezo hivyo.

9. Waombaji wote wa nafasi zilizotangazwa kwa niaba ya Mfuko huo ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili watambue kuwa hawakukidhi vigezo, hivyo wasisite kuomba tena pindi nafasi za kazi zitakapotangazwa.

Bofya hapa kuona ORODHA YA MAJINA 

google+

linkedin

About Author
  • BLOG NAMBA MMOJA KWA MATANGAZO YA AJIRA NA NAFASI ZA KAZI TANZANIA. Soma zaidi

    0 comments:

    POST A COMMENT